Imamu kurefusha du´aa ya Qunuut katika Witr

Swali: Tunatarajia kutuwekea wazi Sunnah katika du´aa ya Qunuut. Je, kuna du´aa maalum? Je, imewekwa katika Shari´ah kurefusha du´aa katika swalah ya Witr?

Jibu: Miongoni mwa du´aa za Qunuut ni ile pamoja vilevile na ile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyomfunza Hassan bin ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhum):

اللهم اهدني فيمن هديت, وعافني فيمن عافيت, وتولني فيمن توليت, وبارك لي فيما أعطيت, وقني شر ما قضيت, فإنك تقضي ولا يقضى عليك, وإنه لا يذلّ من واليتَ, ولا يعزّ من عاديت, تباركت ربنا وتعاليت، لا منجا منك إلا إليك

“Ee Allaah! Niongoze pamoja na wale Uliowaongoza, uniafu pamoja na wale Uliowaafu, Uniangalie pamoja na wale Unaowaangalia, Unibariki katika kile Ulichotoa na Unilinde kutokamana na shari kwa yale Uliyohukumu. Kwani hakika Wewe ndiye mwenye kuhukumu na wala Huhukumiwi. Hakika hatwezeki yule Uliyemfanya mpenzi na wala hapati nguvu yule Uliyemfanya adui. Umebarikika na Umetukuka Mola wetu. Hakuna mahali pa kuokoka kutokamana na Wewe isipokuwa Kwako.”

Imamu yeye anatakiwa kusema:

اللهم اهدنا

“Ee Allaah! Tuongoze… “

kwa dhamira ya wingi. Kwa sababu anajiombea yeye mwenyewe na wale waswaliji walioko nyuma yake. Akileta kitu munasibu ni sawa pia. Lakini haitakiwi kurefusha urefushaji unaowatia uzito maamuma au ukawafanya wakachoka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkasirikia Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) pindi aliporefusha swalah na kumwambia:

“Ee Mu´aadh! Hivi wewe ni mfitini?”[1]

[1] al-Bukhaariy (668) na Muslim (465).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/135)
  • Imechapishwa: 18/06/2017