Imamu kunyanyua sauti katika swalah ya jeneza

Swali: Imamu akisoma kwa suati katika swalah ya jeneza tuseme “Aamiyn” wakati anapomaliza kusema:

وَلاَ الضَّالِّينَ

”… na wala wale waliopotea!”?

Jibu: Hapana, hili halikuwekwa. Ibn ´Abbaas alifanya hili kwa ajili tu ya kuwafunza watu kuwa kunasomwa al-Faatihah. Isitoshe hakunyanyua sauti sana, alinyanyua sauti kwa kiasi cha kumsikia aliye karibu naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-29.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014