Imamu asome Basmalah kwa sauti ya juu kabla ya al-Faatihah?

Swali: Inajuzu kwa imamu kusoma Basmalah kwa sauti ya juu kabla ya kusoma al-Faatihah?

Jibu: Inategemea na madhehebu wanayofuata nchi anayoishi ndani yake. Ikiwa watu wa nchi wanafuata madhehebu ambayo hawasomi Basmalah kwa sauti ya juu, basi asisomi kwa sauti ya juu ili asije kuwachanganya watu. Ama akiwa katika nchi ambayo wanafuata madhehebu yanayosoma Basmalah kwa sauti ya juu, afanye hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (49) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/m-3%20%20-%2012%20-%202%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/10/2018