Imamu asiyekuwa na utulivu


Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya imamu asiyekuwa na utulivu katika swalah yake na khaswa yule ambaye hatuwezi hata kusoma al-Faatihah yote?

Jibu: Ikiwa anayefanya kasoro katika utulivu basi swalah yake haisihi. Uchahe wa utulivu ni mtu atulizane na awe imara mpaka kila kiungo kiweze kurudi mahali pake pamoja na kusema “Subhaan Allaah”. Kuhusu usomaji wa al-Faatihah unatakiwa uisome ijapo imamu pia anaisoma. Ni kitu kilichovuliwa kwa mujibu wa maoni sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 06/03/2021