Swali: Imamu akienda Rak´ah ya tano katika swalah ya Rak´ah nne kwa sababu amesahau kusoma al-Faatihah katika Rak´ah moja wapo na waswaliji hawajui uhalisia wa imamu – je, wamfuate imamu katika hiyo ya Rak´ah au hapana?

Jibu: Kimsingi ni kwamba imamu akienda katika Rak´ah ya tano basi waswaliji wanatakiwa kumzindua. Mwenye kufanya hivo awe ni mtu mwaminifu. Akirudi ni sawa. Vinginevyo wakae chini wakimsubiri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 29/07/2019