Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kugeuza “dhaal” kwenda “zaal” katika al-Faatihah:

صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ

“Njia ya wale Uliowaneemesha.” (01:07)

Jibu: Si sawa. Si sawa kusoma kwa lahja ya isiyokuwa ya kiarabu. Asisome kwa lahja isiyokuwa ya kiarabu na kwenda katika lahja ya kimisri au nyingine. Asisomi kwa lahja nyinginezo. Asome kwa lahja ya kiarabu ambayo Qur-aan imeteremshwa kwayo. Asome kwa lahja ya kiarabu. Asiyeweza kufanya hivo asiwaongoze watu. Haifai kuwa imamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (58) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-14.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020