Imamu anasoma Qunuut katika kila Fajr


Swali: Imamu anasoma Qunuut katika kila swalah ya alfajiri. Mimi naonelea kuwa kitendo hichi ni Bid´ah. Ni lipi la wajibu kwangu? Je, niswali pamoja naye?

Jibu: Ndio, swali pamoja naye. Swali pamoja naye na mfuate. Qunuut ni du´aa. Haya ni madhehebu yake. Fuata madhehebu yake inapokuja katika suala hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (71) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah26-07-1438h%20-%20Copy.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2017