Imamu anasoma du´aa ya kukhitimisha Qur-aan ilihali hakukhitimisha katika Tarawiyh

Swali: Waswaliji walimuuliza imamu ni vipi anaomba du´aa ya kukhitimisha Qur-aan ilihali hukusoma Qur-aan yote katika Tarawiyh wala katika kisimamo cha usiku ambapo akajibu kwa kusema kuwa yeye anasoma Qur-aan katika kisimamo na katika Tarawiyh kisha anaendelea kisomo nje ya swalah ili aweze kuimaliza na akawatuliza ya kwamba anapupia kukhitimisha Qur-aan. Je, imesuniwa kwa mswaliji kuendeleza kisomo nje ya swalah ili aweze kukhitimisha Qur-aan?

Jibu: Hatujui jambo hili kutoka katika Sunnah wala katika matendo mema ya Salaf. Kheri yote inapatikana katika kufuata. ´Ibaadah zimejengeka juu ya ukomekaji na hakuingii Ijtihaad wala kipimo.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (06/90) nr. (21263)
  • Imechapishwa: 23/04/2022