Imamu anaonelea kufupisha kumswalisha maamuma asiyeonelea kufupisha


Swali: Maamuma akiingia pamoja na imamu na huku amenuia kutofupisha katika swalah ya Rak´ah nne. Imamu anaonelea kuwa ni safari. Imamu akatoa salamu pamoja na maamuma ambaye yeye haonelei kufupisha na wote wawili wako katika safari?

Jibu: Ikiwa yeye haonelei kufupisha na imamu anaonelea kufupisha, wakati imamu atapotoa salamu asimame yeye na kukamilisha swalah yake baada ya imamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-01-27.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014