Imamu ametoa salamu baada ya Rakaa´ moja katika Tarawiyh

Swali: Imamu katika swalah ya Tarawiyh akitoa Tasliym baada ya Rakaa´ moja kwa kusahau afanye nini; aifanye Witr au afanye nini pamoja na kuzingatia kuwa maamuma hawakumzindua hadi alipotoa salamu?

Jibu: Imamu akitoa Tasliym baada ya Rakaa´ ya kwanza kisha maamuma wakamkumbusha ni wajibu kwake kusimama na kukamilisha Rakaa´ nyingine moja na asujudu sujudu ya kusahau baada ya kutoa salamu. Haijuzu akaifanya Witr. Kwa sababu hakunuia Witr tokea mwanzo. Lakini kinyume na hilo iwapo imamu atasimama katika swalah ya Tarawiyh katika Rakaa´ ya tatu ambapo watu wakamkumbusha, aendelee au arudi? Ni wajibu kwake kurudi. Akiendelea basi swalah yake ni batili. Ni wajibu kwake kurudi, alete Tashahhud kisha atoe Tasliym. Kisha asujudu sujudu ya kusahau baada ya salamu halafu alete Tasliym.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1623
  • Imechapishwa: 27/05/2018