Imamu amesoma al-Faatihah pekee katika Rakaa´ ya pili katika swalah ya kupatwa kwa jua

Swali: Imamu aliswali swalah ya kupatwa kwa jua na katika Rak´ah ya pili hakusoma isipokuwa al-Faatihah peke yake. Je, swalah yake ni sahihi? Naomba kuwekewa wazi.

Jibu: Swalah yake ni sahihi. Kwa sababu amesoma nguzo ambayo ni al-Faatihah. Pia unatakiwa kutambua kwamba Rukuu´ ya pili katika kila Rak´ah sio wajibu. Imependekezwa. Ile Rukuu´ ya kwanza ndio wajibu na ndio nguzo. Kwa ajili hiyo ndio maana tumesema kuwa Rakaa´ haiwahiwi isipokuwa kwa kuwahi ile Rukuu´ ya kwanza. Kwa sababu ndio nguzo. Kuhusu Rukuu´ ya pili imependekezwa tu. Lakini nitapendelea lau maimamu wataomba wasimamizi wa misikiti ili waweze kubainisha hukumu hizi zilizofichikana kwa wengi wao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/860
  • Imechapishwa: 19/06/2018