Imamu amesema “Allaahu Akbar” badala ya “Samiy´a Allaahu liman hamidah”


Swali: Imamu wetu alisema: الله أكبر “Allaahu Akbar.” badala ya: سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَه “Samiy´a Allaahu liman hamidah” Isitoshe hakwenda Sujuud-us-Sahuw kutokana na ujinga. Ni ipi hukumu ya swalah?

Jibu: Ikiwa alisema hivo kwa kukusudia swalah inabatilika. Ama ikiwa alifanya hivo kutokana na kusahau au ujinga, basi ni lazima kuleta Sujuud-us-Sahuw. Ikiwa alileta Tasliym kabla ya Sujuud-us-Sahuw, basi anatakiwa afanye Sujuud-us-Sahuw baada ya Tasliym. Na ikiwa muda umeshapita mwingi au wudhuu´ wake umetenguka, basi haimuwajibikii kuleta Sujuud-us-Sahuw.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (21) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1434-08-14.mp3
  • Imechapishwa: 20/05/2018