Imamu amesahau Tashahhud ya kwanza na waswaliji wameshaondoka

Swali: Unasemaje juu ya mtu ambaye ameswali Maghrib na akasahau Tashahhud ya kwanza. Hakukumbuka na wala mkusanyiko hawakumkumbusha. Yeye alifikiri kuwa aliikaa katika Tashahhud ya kwanza ambapo akawa ametoa Tasliym kutoka katika swalah na wala hakuna aliyemkumbusha na wala hakusujudu Sujuud-us-Sahw. Baada ya watu kwenda zao akamuuliza muadhini kama aliikaa katika Tashahhud ya kwanza ambapo akamwambia kuwa hakukaa. Ni ipi hukumu katika hali kama hii?`

Jibu: Ikiwa mtu huyu aliyesimama katika Tashahhud ya kwanza alisahau kisha akakumbushwa, ikiwa muda haujapita mwingi, basi alete Sujuud-us-Sahw na wala hakuna neno. Ama ikiwa muda umeshapita mwingi, basi Sujuud-us-Sahw inaanguka na swalah yake ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/878
  • Imechapishwa: 10/08/2018