Imamu amekumbuka kabla ya Tasliym kwamba hana wudhuu´

Swali: Niliwaswalisha watu na sikukumbuka kuwa sina wudhuu´ isipokuwa katika Tashahhud ya mwisho kabla ya Tasliym. Nikakamilisha swalah na sikuwaambia kitu. Je, kipi kinachonilazimu hivi sasa?

Jibu: Ukikumbuka ndani ya swalah kwamba huna wudhuu´, swalah yako na swalah yao ni batili. Ama ukiswali ukamaliza na usikumbuke isipokuwa baada ya kumaliza swalah, swalah yao ni sahihi na swalah yako wewe ni batili. Haijuzu kwako kuendelea ilihali unajua kuwa huna wudhuu´. Ni wajibu kwako kutoka na kuwaeleza kuwa huna wudhuu´. Katika hali hiyo ima wakusubiri na uwaswalishe kuanzia mwanzo au wamteue imamu katika wao awaswalishe. Mtu huyo anatakiwa kuanza swalah mwanzo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (59) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-29-01-1438_0.mp3
  • Imechapishwa: 04/11/2017