Imamu amekumbuka hana wudhuu´ kabla ya Tasliym


Swali: Imamu akikumbuka kuwa hana wudhuu´ kabla ya Tasliym atoke ndani ya swalah au afanye nini?

Jibu: Akikumbuka basi ni lazima kwake kusogea nyuma na amtangulize aliye nyuma yake ijapo ni kabla ya Tasliym na wala asiendelee kuswali.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 07/03/2021