Imamu akhitimishe Qur-aan katika Tarawiyh au asikhitimishe?

Swali: Mimi ni imamu wa msikiti. Nina nia ya kutokhitimisha Qur-aan katika swalah ya Tarawiyh. Lakini baadhi ya watu msikitini wanapendelea, bali wananilazimisha juu ya hilo. Natakiwa niwe na msimamo gani kwao? Nifuate mtazamo wangu au mtazamo wao?

Jibu: Fuata mtazamo wako midhali endapo utawakhitimishia Qur-aan utawarefushia. Kwa sababu iwapo utataka kuchunga Sunnah inapokuja katika idadi ya Rak´ah, basi utatakiwa uswali Rak´ah kumi na moja. Katika kila usiku ukiwasomea juzu moja, itakuwa ngumu kwao. Lakini soma kile kitachokuwa chepesi. Ukikhitimisha Qur-aan kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka mwisho wa mwezi ni jambo zuri. Na usipoweza kufanya hivo sio wajibu. Wewe soma kile kitachokuwa chepesi. Hapa chuoni tangu tuanze kuswali Rak´ah kumi na moja peke yake hatukhitimishi Qur-aan. Isipokuwa tunapoweza kuikhitimisha katika nyusiku za Tahajjud mwishoni mwa mwezi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1378
  • Imechapishwa: 02/12/2019