Swali: Mtu Raafidhwiy akitoa salamu nimuitikie?

Jibu: Ikiwa unajua kama kweli ni Raafidhwiy usimuitikie. Anastahiki kususwa. Hili ni pale unapojua kama kweli ni Raafidhwiy anadhihirisha Bid´ah zake. Ama ikiwa hadhihirishi Bid´ah zake, bali anashirikiana na Ahl-us-Sunnah, anaswali pamoja nao na haonyeshi Bid´ah zake, ataamiliwe kama Ahl-us-Sunnah wengine. Ama ikiwa anadhihirisha Bid´ah zake anastahiki kususwa pamoja na kuendelea kumnasihi huenda Allaah Akamwongoza. Usikate tamaa. Ama akiendelea katika Bid´ah zake anastahiki kususwa.

Swali: Ikiwa kushirikiana kwake na Ahl-us-Sunnah ni kwa njia ya Taqiyyah?

Jibu: Midhali yuko pamoja na Ahl-us-Sunnah asisuswe mpaka pale atapodhihirisha Bid´ah zake. Akizidhihirisha ndio asuswe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah (02)
  • Imechapishwa: 09/08/2020