Imaam al-Fawzaan kufanya kazi ya kuchunga usalama katika benki


Swali: Kuna mtu anafanyia kazi kampuni ya usalama ambayo imempa kazi ya kuchunga benki ilio na ribaa. Inajuzu kufanya kazi huko?

Jibu: Ikiwa anaweza kuhama kwenda sehemu ya kazi nyingine ni bora zaidi na inamtakasia dhimma yake. Vinginevyo anaweza kufanya kazi huko. Kazi yake yeye ni kuchunga benki na mengineyo. Anaweza kuchunga. Majukumu ya benki yako kwa wafanya kazi wao na waasisi wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 03/06/2018