Imaam al-Albaaniy kuhusu kufanya migomo

Swali: Je, inajuzu kwa raia, au baadhi yao, kufanya mgomo wa njaa mbele ya sehemu za watawala na watawala kwa kutaraji kuwatimizia baadhi ya mahitajio yao?

Jibu: Mgomo wa njaa?

Muulizaji: Ndio, mgomo wa njaa kama maandamano na wanasimaa mbele ya sehemu ili…

al-Albaaniy: Hapana, hii ni ada geni na ya kikafiri. Haijuzu kwa waislamu kuitumia kama njia ya kuonyesha kutoridhia kwao baadhi ya mambo yanayotoka serikalini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ibnbaz.se/Artiklarna/101-200/040.html
  • Imechapishwa: 05/09/2020