Imaam Abu Haniyfah kuhusu maneno ya Allaah

Imaam Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) amesema kwenye kitabu chake alichokiita “Fiqh-ul-Akbar” maneno yenye maana:

“Maneno ya Allaah yameandikwa katika misahafu, yanasomwa kwa ndimi, yamehifadhiwa na vifua na yameteremshwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Matamshi yetu juu ya Qur-aan yameumbwa na Qur-aah haikuumbwa. Aliyotaja Allaah katika Qur-aan kuhusu Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Ibliys na Fir´awn pia ni Maneno ya Allaah akiwaelezea. Maneno ya Muusa na ya wengine yameumbwa.

Maneno ya Allaah sio kama maneno ya viumbe. Anajua lakini si kama ujuzi wetu. Anaweza lakini si kama uwezo wetu. Anaona lakini si kama kuona kwetu. Anazungumza lakini si kama kuzungumza kwetu.”

Amesema maneno aina hii.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/178)
  • Imechapishwa: 30/05/2020