Swali: Baadhi ya watu wanaponyanyua mikono yao wakati wa Takbiyrat-ul-Ihraam basi hunyanyua mikono yao hadi kwenye kitovu au juu yake kidogo. Je, kitendo hicho ni sahihi? Ni kipi kinachomuwajibikia mtu akiwa na elimu kisha akamwacha mtu huyu ambaye hakunyanyua mikono yake usawa na mabega au usawa na masikio?

Jibu: Unyanyuaji huo uliotaja haukuwekwa katika Shari´ah. Ukweli wa mambo ni kwamba ni upuuzi wenye kukatazwa. Unyanyuaji uliowekwa katika Shari´ah ni ima hadi kwenye mabega au usawa na ncha ya masikio[1]. Yale mengine yote yenye kupungua juu ya hayo ni mapungufu katika Sunnah, jambo ambalo linatakiwa kukatazwa. Ima anyanyua kikamilifu au aachee kabisa kufanya hivo.

Swali: Ni lazima kwa mtu ambaye ana ujuzi juu ya suala hilo amzindue?

Jibu: Ndio, kanisa.

Swali: Vipi ikiwa ataacha?

Jibu: Akiacha basi amefanya mapungufu. Ataulizwa juu ya hilo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ

“Wakati alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu [akawaambia:] “Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha.”[2]

Katika hali hii kumehitajika ubainifu.

[1] Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Baada ya (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumaliza kisomo alikuwa akinyamaza kidogo. Halafu akiinyanyua mikono yake kama alivyofanya katika Takbiyrat-ul-Ihraam, analeta Takbiyr na kwenda katika Rukuu´.” (Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 112)

[2] 03:187

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (9 B)
  • Imechapishwa: 26/12/2020