Swali: Kuna mtu ameandika makala kwenye gazeti moja ambapo anaomba kuhuisha maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba huku ni kuhuisha Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kumkumbuka na kuhuisha mazao yake. Vilevile anasema kuwa kuna Hadiyth Swahiyh zimekuja kuhusu hilo. Vipi kumraddi huyu?

Jibu: Radd kwa mtu huyu iko wazi. Zipo wapi Hadiyth Swahiyh zilizokuja kuzungumzia juu ya kuhuisha maulidi? Bali ziko wapi Hadiyth dhaifu? Hakuna hata Hadiyth dhaifu juu ya kuhuisha maulidi. Mtu huyu ima ni mjinga au ni muongo na anachotaka ni kuwapaka watu mchanga wa machoni.

Watu wako macho na wamezinduka. Hawadanganyiki kwa maneno kama haya. Bali maneno kama haya yanaonesha ni ujinga au upotevu ulioje alionao aliyoyasema. Anajifedhehesha mbele ya watu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2138
  • Imechapishwa: 12/07/2020