Swali: Inajuzu kumpachika mtu kwa dhati yake ya kwamba ni kafiri?

Jibu: Ndio, inajuzu kwetu kumpachika mtu kwa dhati yake ya kwamba ni kafiri yatapotimia kwake masharti ya ukafiri. Kwa mfano endapo tutamuona mtu anapinga Ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mtu anaruhusu kuhukumiwa kwa hukumu za kikafiri au mtu mtu anaruhusu kuhukumiwa kinyume na yale Aliyoteremsha Allaah na wakati huohuo anasema kuwa ndio bora kuliko Shari´ah ya Allaah. Anafanya yote haya baada ya kufikiwa na dalili. Katika hali hii tunamhukumu kuwa ni kafiri. Zitapopatikana sababu za kufuru na yakatimia masharti na vikwazo vikaondoka, katika hali hii tunamkufurisha mtu kwa dhati yake na tunamlazimisha ima kurudi katika Uislamu au kuuawa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/124-125)
  • Imechapishwa: 25/07/2017