Swali: Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaswalisha Mitume (´alayhim-us-Swalaatu was-Salaam) hali ya kuwa yeye ndiye imamu Yerusalemu Allaah alikuwa amewafufua au ilikuwa ni roho zao?

Jibu: Allaah ndiye anajua zaidi. Muhimu ni kuwa sisi tunaamini hili kama alivyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hatuingii ndani ya maswali haya ilihali hatujui. Tunathibitisha yale aliyothibitisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala hatuingii ndani ya mambo haya. Allaah ni muweza juu ya kila kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (03) http://alfawzan.af.org.sa/node/2046
  • Imechapishwa: 23/10/2016