Ikiwa kaburi ndio lilitangulia basi msikiti ubomolewe


Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali katika msikiti ambao ndani yake kuna kaburi? Je, kuna hukumu tofauti ikiwa kaburi liliingizwa kabla ya kutengeneza msikiti au baada yake?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amewalaani mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni sehemu ya kuswalia.”

Swalah haisihi kuswali ndani ya msikiti ulio na kaburi. Maadamu kaburi liko ndani ya kuta za msikiti. Ama kaburi likiwa nje ya msikiti hakuna neno. Lililo la wajibu inatakiwa kulifukua kaburi ikiwa msikiti ndio ulitangulia. Katika hali hiyo lifukuliwe na kupelekwa sehemu nyingine. Ikiwa kaburi ndio lilitangulia basi msikiti huo ubomolewe na kujengwa sehemu nyingine. Haijuzu kulibakiza kaburi ndani ya msikiti

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 03/04/2018