Swali: Ni lipi la wajibu kwa anayeomba idhini pale ambapo hakupewa ruhusa [ya kuingia] au hakufunguliwa, je, ampe udhuru ndugu yake au ni juu yake kutafuta sababu?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَإِن قِيلَ لَكُمُ ارْجِعُوا فَارْجِعُوا ۖ هُوَ أَزْكَىٰ لَكُمْ

“Mkiambiwa: “Rejeeni’, basi rejeeni. Huo ni utakaso zaidi kwenu.” (24:28)

Arudi pasi na [ndani ya moyo wake] kuwa na kitu kwa ndugu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-11-02.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014