Swali: Baba yetu yuko na dishi/king´amuzi na tumemnasihi kuiondosha. Je, inafaa kwetu kuivunja? Iwapo atatughadhibikia kwa kitendo chetu hichi tunapata dhambi?

Jibu: Ikiwa kuivunja kwenu kutamkasirisha lakini hatonunua nyingine badala yake, basi ivunjeni ijapokuwa atakasirika. Mioyo iko mikononi mwa Allaah (´Azza wa Jall). Huenda kweli akakasirika lakini hata hivyo hatimaye akaridhika. Ama ikiwa mtaivunja leo huko baadaye atanunua nyingine, msiivunje. Kwa sababu itakuwa ni kuharibu pesa bila ya faida yoyote. Lakini hata hivyo ikiwa mnaishi naye katika nyumba moja msikae naye wakati atapokuwa anatazama mambo ya haramu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1461
  • Imechapishwa: 11/01/2020