Swali 300: Je, mwanamke akiswali swalah ya ijumaa inadondoka kwake swalah ya Dhuhr?

Jibu: Mwanamke akiswali pamoja na imamu swalah ya ijumaa basi inamtosha kutokamana na Dhuhr. Hivyo haijuzu kwake kuswali Dhuhr ya siku hiyo. Ama akiswali peke yake basi haifai kwake kuswali isipokuwa Dhuhr na asiswali ijumaa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 115
  • Imechapishwa: 12/10/2019