Swali: Ni upi msimamo wa Shaykh Ibn Baaz na Shaykh al-Albaaniy (Rahimahuma Allaah) juu ya jumuiya ya Ihyaa´ at-Turaath?

Jibu: Shaykh al-Albaaniy ni mwenye kujiweka nayo mbali kabisa. Shaykh Ibn Baaz aliwakataza baadhi ya mambo. Hizbiyyuun ni wenye kutatiza. Wao huwaendea wale Mashaykh wa Ahl-us-Sunnah watukufu ambao wana uaminifu kwao na wanasema: “Ee Shaykh! Hakika Allaah Ametuhakikishia kheri nyingi juu ya jambo hili na tumeenda mpaka Afrika – ukweli wa mambo Afrika wamefarikanisha Umoja wa Waislamu – tumeenda Indonesia, Pakistan na kadhalika. Hivyo Shaykh anawasadikisha. (Shaykh al-Albaaniy) alimradi ´Abdur-Rahmaan ´Abdul-Khaaliq. Na mimi nina uhakika ya kwamba Shaykh (Ibn Baaz) atakapobainikiwa na jambo lao, atajiweka nao mbali.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3661
  • Imechapishwa: 14/07/2020