Iheshimu Ramadhaan na usifungue mgahawa Ramadhaan!


Swali: Ndugu yangu anamiliki mgahawa katika nchi isiyokuwa ya Kiislamu. Je, afungue mgahawa mchana wa Ramadhaan au asifanye hivo pamoja na kuzingatia ya kwamba katika nchi hiyo wapo pia waislamu?

Jibu: Hapana. Asifungue mgahawa mchana. Huu ni muonekano ambao unapingana na mfumo wa Uislamu. Mchana hakuna kula wala kunywa. Auheshimu mwezi. Asifungue hata kama ni katika nchi ya makafiri. Kwa sababu yeye ni muislamu. Anatakiwa kuuwakilisha Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=uV5S807lDYg
  • Imechapishwa: 22/05/2018