Idhini ya mtawala kwenda katika Jihaad


Swali: Je, inajuzu kutoka kwenda katika Jihaad bila ya idhini ya mtawala ikiwa wazazi wameridhia?

Jibu: Jihaad pamoja na nani? Ni kiongozi yupi ambaye wewe unapigana Jihaad chini ya uongozi wake? Vilevile nchi zina mikataba. Ni lazima upate idhini ya mtawala ya kwenda katika nchi hiyo. Mambo haya yana misingi yake. Sio mambo ya vurugu. Mtawala akikupa idhini na vilevile wazazi wako wakakupa idhini na wewe ukawa na uwezo, ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_14.mp3