Swali: Kuna chaneli inayorusha kutoka nje ya Saudi Arabia. Mengi yaliyomo ni nyimbo na muziki. Lakini wameweka kitu katika fatwa ambapo watu wakawa wanasikiliza. Ni ipi hukumu ya kuisikiliza pamoja na kuzingatia kwamba kuna balaa hilo?

Jibu: Kwa hali yoyote ya kwamba chaneli zinaweka kheri na shari. Ikiwa unaiamini nafsi yako kwamba unaweza kujizuia na hiyo shari na ukasikiliza mambo ya kheri ni sawa. Kwa sababu redio au TV hii ni jambo liko mikononi mwako. Ukitaka unaweza kuifunga na ukitaka unaweza kuifungua. Ikiwa kunapita mambo ya kheri ni sawa ukasikiliza. Kwa sharti ujiaminishe nafsi yako. Kwa sababu baadhi ya watu wanasema kuwa wanataka kusikiliza fataawaa na taarifa ya khabari. Lakini shaytwaan anawavuta kidogo kidogo mpaka mwishowe wanasikiliza mambo ya haramu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1735
  • Imechapishwa: 31/08/2020