Idara ya masomo imewaamrisha wanafunzi wote kunyoa kipara

Swali: Kumekuja amri kutoka idara ya masomo ikiwalazimisha wanafunzi kunyoa nywele za kichwani mwao. Lakini kubakiza nywele ndio Sunnah. Ni ipi taaliki yako juu ya hilo?

Jibu: Kuna wasaa katika jambo hili. Kunyoa nywele sio lazima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah walikuwa wakifuga nywele za vinywani mwao. Lakini kunyoa pia inafaa. Kufuga ni jambo limesuniwa kwa jumla. Lakini ikiwa wahusika wa chuo wamefanya hivo kwa sababu inayokubalika katika Shari´ah, pengine ili wanawake wasije kufitinishwa nao au wenyewe wakafitinishwa nao au kwa sababu nyenginezo  walizoziona zilizo na manufaa kwa wanafunzi hakuna neno. Wao ndio wanajua zaidi. Kama wameona kuwa jambo hilo lina manufaa basi wanapaswa kuitikia. Kwani kufanya hivo ni katika kuwatii watawala katika mema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4283/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%85%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%B7%D9%84%D8%A7%D8%A8-%D8%A8%D8%AD%D9%84%D9%82-%D8%B1%D9%88%D9%88%D8%B3%D9%87%D9%85
  • Imechapishwa: 29/05/2020