Swali: Kuna idadi ngapi ya Manabii na Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam)?

Jibu: Hakuna anayejua idadi yao. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ

“Hakika Tumewapeleka Mitume kabla yako; miongoni mwao wako Tuliokusimulia na miongoni mwao wako ambao hatukukusimulia.” (40:78)

Wanaojulikana katika wao ni wale waliotajwa katika Qur-aan au wamesihi kutajwa katika Sunnah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/195)
  • Imechapishwa: 23/08/2020