Swali: Je, inafaa kumsalimia mtu anayefanya Bid´ah?

Jibu: Ikiwa mzushi analingania katika Bid´ah yake na kuna manufaa katika kule kumsusa, basi usimsalimie. Lakini ikiwa hakuna manufaa katika kule kumkata, basi msalimie. Ikiwa kumsusa kwako mtu anayefanya Bid´ah, basi atakufanya wewe ni adui na  kuwachochea watu dhidi yako. Hakuna faida ya kumkata. Lakini ikiwa kuna faida katika kumkata, kwa njia ya kwamba mtu huyo ni mwenye ushawishi kwa watu wake na ikiwa atamsusa basi kutamfanya mzushi huyo kujirejea, hapo hakuna neno.

Hii ni kanuni yenye kuenea. Haijuzu kumkata kila mtenda dhambi ambayo haijafikia kiwango cha ukafiri isipokuwa ikiwa katika kufanya hivo kuna manufaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (145 B) Tarehe: 1417-08-02/1996-12-12
  • Imechapishwa: 02/09/2021