Ibn ´Uthaymiyn wanawake kubadilisha rangi ya nywele zao

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuzipaka nywele zake rangi nyingine isiyokuwa nyeusi kama mfano wa rangi ya chokleiti na nyekundunyekundu?

Jibu: Kimsingi katika jambo hili ni kufaa. Isipokuwa ikifikia katika kiwango cha kujifananisha na vichwa vya wanawake wa kikafiri, makahaba, watenda dhambi. Katika hali hiyo itakuwa haramu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/118)
  • Imechapishwa: 28/06/2017