Ibn ´Uthaymiyn wafanya matabano wanaowasomea watu Ruqyah kwa njia ya simu

Swali: Kuna mtu yuko katika nchi jirani ya Saudi Arabia ananipigia simu na kunambia jina langu ni fulani mama yako jina lake ni fulani na wakati mwingine anaweza kukwambia ugonjwa ulionao kama ni ya wa kinafsi, uchawi au kama ni ugonjwa wa kikaboni. Je, hili linajuzu?

Jibu: Vipi litajuzu? Mtu hajamuona mgonjwa ambapo mgonjwa huyo akamweleza na kuhusu maradhi yake na anamwambia kwamba ana uchawi, jini au kijicho. Je, huyu anayajua mambo yaliyofichikana? Ni mchawi au ni anatumia majini. Hatujui. Kwa hali yoyote ni sawa kufanya hivo. Hili si jambo la sawa. Lakini akijua kuwa fulani ana uwezo wa kuliondosha jini kwa njia ya kwamba anaweza kumsomea yule mgonjwa na kuliondosha jini, huyu inafaa kwako kumpelekea huyo mgonjwa akamsomea mpaka atokwe na kile kilichomwingia. Sisi hatupingi kuwa mmoja katika watu anaweza kuliondosha jini kutoka kutoka kwa mwanadamu. Hili ni jambo la uhalisia. Hili ni jambo limekuja katika Sunnah na maimamu wakalitendea kazi. Shaykh-ul-Islaam alikuwa hodari wa jambo hili. Alikuwa akiletewa mgonjwa ambaye ameingiwa na jini na anamsomea ambapo anampambana naye na mwishowe anaamua kutoka nje.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1306
  • Imechapishwa: 24/10/2019