Ibn ´Uthaymiyn visa vya uongo ili kuwachekesha watu


Swali: Ni yapi maoni yako juu ya yale yanayotokea katika vikao vya watu vya kibinafsi na vya kijumla katika mizaha na visa vizuri kwa lengo la kuwasahilishia watu pamoja na kuzingatia ya kwamba mara nyingi vinakuwa sio ya vya ukweli na si sahihi? Hoja yao ni kwamba wasikilizaji wanajua kuwa sio vya kweli.

Jibu: Visa vya uongo na visivyokuwa na asli vinaingia ndani ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ole wa yule mwenye kuzungumza akadanganya ili awachekeshe watu! Ole wake! Ole wake!”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekariri hilo mara tatu. Hii ni dalili yenye kuthibitisha kuwa ni haramu. Mwenye kuelezea kisa cha uongo ili kutaka kuwachekesha watu, anapata dhambi na anaingia katika matishio haya – ulinzi unatakwa kutoka kwa Allaah.

“Ole wa yule mwenye kuzungumza akadanganya ili awachekeshe watu! Ole wake! Ole wake!”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (13)
  • Imechapishwa: 01/10/2017