Ibn ´Uthaymiyn utoko unaotoka kwenye tupu ya mwanamke 02

Swali: Je, inasihi kwa mwanamke kuswali swalah mbili kwa wudhuu´ mmoja au ni wajibu kutawadha wakati wa kutaka kuswali kila swalah ya faradhi kwa vile utoko unawatoka sana wanawake? Tumesikia fatwa kutoka kwako kuhusu utoko unaomtoka mwanamke. Jengine ni kwamba utoko huu unakuwa msafi au najisi unapoingia ndani ya nguo? Tunaomba kuwekewa wazi hilo kwa upambanuzi. Kwani jambo hili linawatatiza watu wote.

Jibu: Utoko huu wanaokuwa nao wanawake ni msafi. Isipokuwa ikiwa kama ni mkojo. Mkojo unajulikana kwani una harufu mbaya na rangi maalum. Lakini utoko huu wa kimaumbile na wa kawaida ni msafi. Unapoingia ndani ya nguo au mwilini hanajisiki mtu. Lakini hata hivyo unachengua wudhuu´. Kwa msemo mwingine ni kwamba mwanamke huyu asitawadhe kwa ajili ya kuswali swalah ya faradhi isipokuwa baada ya kuingia wakati wa swalah. Vivyo hivyo anapotaka kuswali swalah za sunnah. Anaweza kukusanya kati ya swalah mbili; Dhuhr na ´Aswr na Maghrib na ´Ishaa ikiwa anapata uzito wa kutawadha kunapoingia wakati wa kila swalah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1245
  • Imechapishwa: 24/09/2019