Ibn ´Uthaymiyn tafsiri ya Qur-aan ya mwanafunzi kuanza nayo

Swali: Ni vitabu vipi ambavyo mwanafunzi ataenda navyo daraja kwa daraja katika tafsiri ya Qur-aan wakati anapoanza kutafuta elimu? Ni yepi maoni yako juu ya Zubdat-ut-Tafaasiyr? Je, inaendana na yule anayeanza kutafuta elimu au haendani nae?

Jibu: Ninavyoona tafsiri ya Qur-aan ambayo ni rahisi kwa yule mwanafunzi anayeanza ni tafsiri ya Qur-aan ya Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Sa´diy. Maneno yake yako wazi, usulubu wake unaeleweka na asiyekuwa msomi na ambaye ni msomi. Katika baadhi ya Aayah kuna faida ambazo huwezi kuzipata kwenye tafsiri zengine. Naona kuwa ndio tafsiri bora zaidi ambayo mtu anaweza kuanza nayo inapokuja katika mada ya tafsiri ya Qur-aan.

Kuhusu tafsiri ya al-Jalaalayn ni kweli kwamba ni fupi. Lakini tafsiri ya al-Jalaalayn inahitajia mtu ambaye ni msomi. Kuna mambo ambayo hayawezu kutatuliwa isipokuwa tu na mwanafunzi ambaye ni mwenye nguvu.

Ama kuhusu Zubdat-ut-Tafaasiyr mimi sijaisoma na wala hata sijui ni nani mtunzi wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (31)
  • Imechapishwa: 28/10/2017