Ibn ´Uthaymiyn stesheni za petroli zinazotawanya kadi kwa ajili ya ofa

Swali: Jambo lililoenea baina ya stesheni za petroli ni kwamba wanatawanya kadi ambayo imeandikwa kwamba ukijaza gari lako kwa kiasi cha lita 500 za petroli, basi wanakupa ofa ya lita 40. Hilo linafanyika kila wakati ambapo unapojaza gari lako basi unapewa kadi kwa kiasi cha thamani ya ile petroli uliyojaza. Baadaye unapokamilisha kile kiwango kilichopangwa unapewa lita 40. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hakuna neno stesheni za petroli wakawa karatasi au ubao ulioandikwa kwamba yule mwenye kufikisha kiwango kadhaa cha petroli, basi anapewa tuzo. Hili linafaa. Lakini kwa sharti bei yake ya mafuta iwe ileile kama iliyoko kwa watu wengine. Asizidishe. Kwa sababu mnunuzi hivi sasa huenda ni mwenye kusalimika au mwenye kupata faida. Hapungukiwi na kitu. Ama ikiwa atazidisha thamani ya petroli, kwa njia ya kwamba wengine wanauza bei ya mafuta pesa 10 na yeye anauza 20, katika hali hii haifai. Kwa sababu katika hali hii yule mteja anakuwa ni mwenye kubahatisha na hii ndio kamari.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1294