Swali: Ni ipi hukumu ya kujinasibisha na as-Salaf as-Swaalih na mtu kusema kwamba yeye ni Salafiy inapokuja katika ´Aqiydah?

Jibu: Kujinasibisha na as-Salaf as-Swaalih ni wajibu. Kwa sababu as-Salaf as-Swaalih ni wale waliokuwa wakifuata yale aliokuwa akifuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ama kusema kwamba yeye ni “Salafiy”, kama anakusudia kuanzisha kipote au kujinasibisha na kipote, basi tunapiga vita vipote. Tunaona kuwa Ummah wa Kiislamu wanatakiwa kuwa Ummah kitu kimoja kwa mujibu wa njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.

Na kama anakusudia kwa msemo wake “mimi Salafiy” ya kwamba yeye anawafuata Salaf pasi na kukusudia kuanzisha kipote kwa ajili ya kuwashambulia wale wanaokwenda kinyume naye, hii ni haki. Sote ni Salafiyyuun! Sote tunamuomba Allaah atufishe juu ya njia ya Salaf. Tunamuomba Allaah hilo.

Ama kuanzisha kipote kwa jina “Salafiy”, kipote kingine kwa jina “al-Ikhwaan”, kingine kwa jina “Tabliyghiy” na kadhalika sioni kuwa inafaa kufanya hivo. Je, Maswahabah walitofautiana namna hii? Hapana. Mwenye hoja kinyume na hii ailete.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Haram al-Madaniy (53)
  • Imechapishwa: 13/02/2019