Ibn ´Uthaymiyn “Natamani lau ningelikuwa najua kingereza”

Swali: Inajuzu kufanya ghushi kwenye lugha ya kingereza ambayo wewe umeikataza?

Jibu: Kwanza mimi sijakataza lugha ya kingereza. Mimi natamani ningekuwa najua lugha ya kingereza ili niwalinganie kwa kingereza wale wasiojua lugha ya kiarabu. Bali nilisema kuwa kujifunza nayo inaweza kuwa aidha faradhi kwa baadhi ya watu au faradhi kwa watu wote. Lakiinia hata hivyo nilichokisema ni kwamba: miongoni mwa makosa tunayoyakemea ni sisi kuwafunza wana wetu wadogo wenye miaka mitano au misita kingereza ilihali hawajui kiarabu. Hili ndilo tunalolikemea. Ama kujifunza kingereza ikiwa kuna manufaa ya kufanya hivo ni sawa.

Kuhusu kufanya ghushi ambaye atafanya ghushi katika somo la lugha ya kingereza ni wajibu kwa mwalimu kumfelisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (15)
  • Imechapishwa: 19/11/2017