Ibn ´Uthaymiyn namna ya kugawanya kati ya saa ya kwanza mpaka ya mwisho siku ya ijumaa

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayeenda katika ile saa ya kwanza, basi ni kama ambaye amekurubisha ngamia. Mwenye kwenda katika ile saa ya pili ni kama ambaye amekurubisha ng´ombe. Mwenye kwenda katika ile saa ya tatu ni kama ambaye amekurubisha kondoo dume wa pembe. Mwenye kwenda katika ile saa ya nne ni kama ambaye amekurubisha kuku. Mwenye kwenda katika ile saa ya tano ni kama ambaye amekurubisha yai.”

Saa hizi zinahesabiwa kuanzia pale ambapo jua linapochomoza halafu unagawanya mara tano kuanzia pale jua linapochomoza mpaka pale imamu anapokuja. Ni mamoja muda ukawa mrefu au mfupi. Kwa sababu muda unatofautiana kati ya kipwa na masika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1717
  • Imechapishwa: 22/04/2020