Ibn ´Uthaymiyn na Ibn Baaz kuhusu kuwatangazia watu kupatwa kwa jua

Swali: Je, inafaa kwa imamu kuwatangazia walioko nyuma yake juu ya kukutana kwa ajili ya kupatwa kwa jua pale ambapo wataalumu wa nyota watasema kuwa jua litapatwa saa fulani kwa lengo ili wapate kuhudhuria au asiwaeleze?

Jibu: Mimi naonelea kuwa asiwaeleze na wala asieneze khabari pale atapozijua. Watu wakitangulia kujua hawatolitilia umuhimu mkubwa na watafikiria ni kama mwezi mkubwa unapochomoza. Kupatwa kwa jua ni jambo la kuogopesha na kukhofisha. Swalah yenyewe ni ya kuogopesha. Sio kama swalah ya ´Iyd ambayo ni swalah ya furaha na kufurahika ili mtu aweze kuitangaza. Kuzificha khabari za kupatwa kwa jua ni bora zaidi kuliko kuzitangazia. Hivi ndivyo ninavoonelea juu ya masuala haya. Pia ndivyo anavyoonelea Shaykh wetu ´Abdul-´Aziyz bin Baaz. Hapana shaka ndio bora zaidi. Kwa ajili hii utawaona watu wanakuja kuswali swalah ya kupatwa kwa jua kama vile wanavyokuja kuswali swalah ya ´Iyd. Kumepatikana kupatwa kwa jua wanakuja kuswali. Lakini hutoona woga mkubwa ambao sisi tulikutana nao. [Hapo kabla] watu walikuwa wanakuja misikitini wepesi na huku wakilia. Utasikia msikitini vilio vitupu. Ama hii leo utaona ni kama vile mwezi wa siku ya ´Iyd ambapo umechomoza na watu wamekuja kuswali. Kwa ajili hii naona kuwa isitangazwe na mtu akipata taarifa asiieneze ili watu waje hali ya kushangaa na wapatwe na woga na kumwogopa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/857
  • Imechapishwa: 19/06/2018