Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuwakusanya watu wa nyumbani wanawake na akawaswalisha swalah ya jeneza juu ya maiti yao kwenye nyumba hiyo?

Jibu: Ndio. Hakuna neno mwanamke akaswalia jeneza. Ni mamoja akaswali msikitini pamoja na watu wengine au akamswalia nyumbani ambapo maiti kafia. Wanawake hawajakatazwa kumswalia maiti. Walichokatazwa ni kuyatembelea makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi na wale wenye kuyafanya kuwa ni mahali pa kuswali na kuyaweka mataa. Hili linahusiana na pale atapokusudia matembezi. Endapo hatokusudia matembezi, kwa mfano ameenda katika haja zake na tahamaki akapita makaburini, haina neno akasimama, akawatolea Salaam waliomo ndani ya makaburi na akawaombea du´aa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa´ ash-Shahriy (01)
  • Imechapishwa: 08/09/2020