Ibn ´Uthaymiyn msafiri kuswali Maghrib nyuma ya mkazi anayeswali ´Ishaa

Swali: Nimenuia mkusanyiko wa kuchelewesha nitapofika Makkah. Nimefika wakati wa swalah ya pili. Nifanye nini?

Jibu: Ingia nao katika swalah ya ´Ishaa na wewe uweke nia ya Maghrib. Ukiingia katika Rak´ah ya kwanza pale ambapo imamu atasimama katika Rak´ah ya nne, wewe huwezi kumfuata. Katika hali hii ufanye nini? Ikaa chini na usome Tashahhud na utoe salamu na halafu uingie pamoja na Imamu katika yaliyobakia katika swalah ya ´Ishaa. Ukiingia na Imamu katika Rak´ah ya pili, toa salamu pamoja naye. Ukiingia naye katika Rak´ah ya tatu, baada ya salamu utaswali Rak´ah moja. Ukiingia naye katika Rak´ah ya nne, baada ya yeye kutoa salamu utaswali Rak´ah mbili. Hii ndio kauli sahihi zaidi iliyosemwa juu ya masuala haya na vilevile ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 03
  • Imechapishwa: 23/09/2020