Ibn ´Uthaymiyn mgonjwa wa pumu kutumia sprei mchana wa Ramadhaan


Swali: Dawa dhidi ya uzito wa kupumua kwa mfungaji inamfunguza?

Jibu: Sprei hii ambayo anatumia ikiwa haifika tumboni, basi katika hali hii tunasema kwamba hakuna ubaya kwako kutumia sprei hii ilihali umefunga. Hufungui kwa kufanya hivo. Kwa sababu ni kama tulivosema kwamba hakuna chembe inayoingia tumboni. Ni kitu ambacho mtu anajipulizia na kinaondoka. Hakuna kitu kinachofika tumboni mpaka tuseme kwamba ni miongoni mwa mambo yanayofunguza. Kwa hivyo inafaa kwako kutumia ilihali umefunga. Swawm haiharibiki kwa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=84940
  • Imechapishwa: 20/05/2018