Ibn ´Uthaymiyn kwamba ni lazima kwa watu wote wawe Salafiyyuun

Swali: Kumezuka kikosi maalum kati ya waislamu kwa jina ”Salafiyyuun”. Jina hili halitumiki kwa waislamu wengine. Ikiwa Uislamu na Salafiyyah ni kitu kimoja na kwamba hakuna tofauti kati ya ”Salafiy” na ”muislamu”, kama ambavo ndani ya Uislamu wako waislamu wenye msimamo, watenda madhambi na wazushi, je, tunaweza kusema kuwa kuko Salafiy ambaye ni mtenda maasi na mzushi? Kwa njia ya kwamba tunaweza kusema kuwa yuko msanii ambaye ni muislamu, lakini msanii huyu tunaweza kusema kuwa ni Salafiy?

Jibu: Kitu cha kwanza ni kwamba tunapaswa kutambua kuwa ”Salafiy” haikukomeka juu ya kikosi maalum. Kila ambaye ni mwenye kushikamana na madhehebu ya Salaf basi huyo ni Salafiy. Huyu ni Salafiy ni mamoja ametangulia hapo kabla au amekuja nyuma. Ama kulifupiza juu ya kundi maalum na kusema kwamba hao ndio Salafiyyuun na wengine ni watumiaji akili, ni kosa. Lakini inatakiwa kutambua kwamba wako wanachuoni ambao wamemili zaidi katika upande wa kutumia akili na wengine wamemili zaidi katika upande wa Shari´ah. Kwa ajili hiyo utaona katika vitabu vya Fiqh pindi wanapowataja Hanafiyyah basi wanawaita kuwa ni ”Ahl-ur-Ray´”, wafuasi wa maoni, kwa sababu wako ambao wanafuata dalili na wengine wanafuata kipimo.

Elewa kanuni hii: Salafiy ni yule mtu ambaye ameshikamana na madhehebu ya Salaf. Haitumiki juu ya kikundi maalum. Haijuzu kuwagawanya watu na kusema hawa ndio Salafiyyuun na hawa wengine ni wenye kutumia akili na mfano wa hayo. Salafiy ni yule mwenye kushikamana na madhehebu ya Salaf katika ´Aqiydah, maneno na vitendo, pasi na kujali yuko mahali gani. Si sahihi kuwagawanya waislamu na kusema kuwa hawa ni wenye kutumia akili, Salafiyyuun na mfano wa hayo. Ni lazima kwa watu wote wawe Salafiyyuun. Yasifanywe kuwa ni mambo ya kivyama, bali ni kwa sababu ndio haki:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

“Wale waliotangulia wa mwanzo [katika Uislamu] miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema – Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye.”[1]

[1] 09:100

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (220 B)
  • Imechapishwa: 28/06/2020