Ibn ´Uthaymiyn kutumia vidonge vya kuzuia hedhi kwa ajili ya Ramadhaan


Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kutumia vidonge vya kuzuia hedhi katika Ramadhaan?

Jibu: Kile ninachoona ni kwamba mwanamke asitumie vidonge hivi, si katika Ramadhaan wala kipindi kingine. Kwa uthibitisho wa madaktari imethibiti kwamba vidonge hivi ni vyenye kudhuru mfuko wa uzazi, mishipa na damu. Kila kitu chenye kudhuru kimekatazwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna madhara wala kudhuriana.”[1]

Nimepata khabari kwamba wanawake wengi ambao wanatumia tembe kama hizi ada yao huvurugika na kubadilika ambapo matokeo yake wanawachokesha wanazuoni. Kwa ajili hiyo nawashauri wasitumie vidonge hivi kwa hali zote.

[1] Ibn Maajah (2340-2341). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaami´” (7517).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/268-269)
  • Imechapishwa: 03/05/2021